Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. HE-2944

Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنِ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: أَمَرَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِسَبْعٍ، وَنَهَانَا عَنْ سَبْعٍ: أَمَرَنَا بِعِيَادَةِ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعِ الْجَنَازَةِ، وَتَشْمِيتِ الْعَاطِسِ، وَإِبْرَارِ الْقَسَمِ، أَوِ الْمُقْسِمِ، وَنَصْرِ الْمَظْلُومِ، وَإِجَابَةِ الدَّاعِي، وَإِفْشَاءِ السَّلَامِ، وَنَهَانَا عَنْ خَوَاتِيمَ -أَوْ عَنْ تَخَتُّمٍ- بِالذَّهَبِ، وَعَنْ شُرْبٍ بِالْفِضَّةِ، وَعَنِ الْمَيَاثِرِ، وَعَنِ الْقَسِّيِّ، وَعَنْ لُبْسِ الْحَرِيرِ وَالْإِسْتَبْرَقِ وَالدِّيبَاجِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Baraa bin Azib radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alituamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo saba, na akatukataza mambo saba: Alituamrisha kumtembelea mgonjwa, na kusindikiza jeneza, na kumuombea mwenye kupiga chafya, na kukiepusha kiapo au kumuepusha (na tuhuma) aliyeapa, na kumnusuru aliyedhulumiwa, na kuitika wito wa mwenye kualika (au kuita), na kutoa salamu, na akatukataza kuvaa pete za dhahabu, na kunywa katika vyombo vya madini ya fedha, na kukalia matandiko ya hariri, na kuvaa kassi (nguo iliyotengenezwa kwa katani na hariri) na kuvaa hariri nyepesi na hariri nzito na dibaji.

English translation

Al-Barā’ ibn ‘Āzib (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) commanded us with seven and forbade us from seven: He commanded us to visit the sick, to follow the funeral, to say Tashmīt to the sneezer, to fulfill the oath, or the one making an oath, to support the oppressed, to respond to the inviter, and to spread the greeting of peace. He forbade us from rings—or from wearing rings—of gold, from drinking in silver, from Mayāthir, from Qassiy, and from wearing silk, Istabraq, and Dībāj.

Maelezo

Aliwaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake waislamu mambo saba na akawakataza mambo saba; yale aliyowaamrisha ni: La kwanza: Kumtembelea mgonjwa. La pili: Kusindikiza jeneza na kushiriki katika kumswalia na kumzika, na kumuombea dua. La tatu: Kumuombea dua aliyepiga chafya na akamhimidi Mwenyezi Mungu, kwa kumuambia: Yar-hamukallaah (Akuhurumie Mwenyezi Mungu). La nne: Kumuepusha aliyetoa kiapo na kumuamini, yaani ikiwa litaapiwa jambo hali yakuwa unauwezo wa kumuepusha na tuhuma basi fanya hivyo; ili usimpelekee kulipa kafara kwa kiapo chake. La tano: Kumsaidia aliyedhulumiwa, kwa kumtetea na kuyazuia yanayotokea kwake miongoni mwa dhulma, kwa kadiri ya uwezo. La sita: Kumuitikia mwenye kualika katika walima wa chakula, kama walima wa harusi, au akika, au kinginecho. La saba: Kutangaza utoaji wa salamu na kuuneza na kujibu pia. Na aliyoyakataza ni: La kwanza: Kuvaa pete za dhahabu na kujipamba nazo. La pili: Kunywa kwa kutumia vyombo vya fedha. La tatu: Kukaa katika matandiko, nayo ni magodoro ambayo huwekwa juu ya mgongo wa farasi, na juu ya ngamia, yaliyotengenezwa kwa hariri. La nne: Kuvaa nguo iliyotengenezwa kwa katani ikachanganywa na hariri, na huitwa (Qassi). La tano: Kuvaa hariri. La sita: Kuvaa hariri nzito. La saba: Kuvaa dibaji, nayo ni: Aina bora zaidi ya hariri na ghali zaidi.

Faida

  • Kumebainisha sehemu katika haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu.
  • Asili ni kuwa kila amri zinazokuja katika sheria au makatazo zinawahusu wanaume na wanawake, isipokuwa yaliyofanywa kuwa maalumu kwa wanaume au wanawake.
  • Hadithi nyingine zimeonyesha juu ya kumkataza mwanamke kusindikiza jeneza.
  • Zimeonyesha hadithi nyingine kufaa kuvaa dhahabu na hariri kwa mwanamke.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)