Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 2616

Hakika umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قُلْت يَا رَسُولَ اللَّهِ! أَخْبِرْنِي بِعَمَلٍ يُدْخِلُنِي الجَنَّةَ وَيُبَاعِدْنِي مِنْ النَّارِ، قَالَ: «لَقَدْ سَأَلْتَ عَنْ عَظِيمٍ، وَإِنَّهُ لَيَسِيرٌ عَلَى مَنْ يَسَّرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ: تَعْبُدُ اللَّهَ لَا تُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا، وَتُقِيمُ الصَّلَاةَ، وَتُؤْتِي الزَّكَاةَ، وَتَصُومُ رَمَضَانَ، وَتَحُجُّ البَيْتَ، ثُمَّ قَالَ: أَلَا أَدُلُّكَ عَلَى أَبْوَابِ الخَيْرِ، الصَّوْمُ جُنَّةٌ، وَالصَّدَقَةُ تُطْفِئُ الْخَطِيئَةَ كَمَا يُطْفِئُ المَاءُ النَّارَ، وَصَلَاةُ الرَّجُلِ مِنْ جَوْفِ اللَّيْلِ، ثُمَّ تَلَا: {تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ} حَتَّى {بَلَغَ يَعْمَلُونَ}، ثُمَّ قَالَ: أَلَا أُخْبِرُك بِرَأْسِ الأَمْرِ وَعَمُودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ، فَقُلْتُ: بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: رَأْسُ الأَمْرِ الإِسْلَامُ، وَعَمُودُهُ الصَّلَاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهَادُ، ثُمَّ قَالَ: أَلَا أُخْبِرُك بِمِلَاكِ ذَلِكَ كُلِّهِ، فقُلْت: بَلَى يَا رَسُولَ اللَّه! فَأَخَذَ بِلِسَانِهِ وَقَالَ: كُفَّ عَلَيْك هَذَا، قُلْت: يَا نَبِيَّ اللَّهِ! وَإِنَّا لَمُؤَاخَذُونَ بِمَا نَتَكَلَّمُ بِهِ، فَقَالَ: ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ وَهَلْ يَكُبُّ النَّاسَ عَلَى وُجُوهِهِمْ أَوْ قَالَ عَلَى مَنَاخِرِهِمْ إلَّا حَصَائِدُ أَلسِنَتِهِمْ»!

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hebu nieleze amali itakayoniingiza peponi na kuniweka mbali na Moto, akasema: "Hakika umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu: Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu bila kumshirikisha na chochote, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhiji. kisha akasema Mtume: Je, nikujulishe milango ya kheri? Funga ni kinga, na sadaka inaondosha madhambi kama maji yanavyo uzima moto, na swala ya mtu katikati ya usiku, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu: "Mbavu zao zinaachana na vitanda..." mpaka alipofikia mwisho wa aya "wanayoyatenda". Kisha akasema Mtume: Je nikueleze kichwa cha mambo yote na nguzo yake na kilele chake? Nikajibu ndio ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: kichwa cha mambo yote ni Uislamu, na nguzo yake ni Swala, na kilele chake ni Jihadi. Kisha akasema: Je nikujulishe kinachoyahifadhi na kuyatunza matendo hayo? Nikasema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akaushika ulimi wake kisha akasema: Zuia ulimi wako, nikamuuliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je tutahesabiwa kwa kila tunacho kizungumza? Akasema: Akukose mama yako, hakuna kitakacho waingiza watu wengi motoni kama maneno wanayoyazungumza."!

English translation

Mu‘ādh ibn Jabal (may Allah be pleased with him) reported: I said: O Messenger of Allah, tell me of an action that lets me enter Paradise and keep me away from Hellfire. He said: "You have asked about something grave, but it is easy for whomever Allah makes it easy for. Worship Allah, without associating anything with Him, offer the prayer, pay Zakah, fast Ramadan, and perform Hajj. Then, he said: Shall I not guide you to the gates of goodness? Fasting is a shield, charity extinguishes sins as water extinguishes fire, and a man's prayer in the middle of night. Then, he recited: {Their sides forsake their beds} until he reached {what they used to do.} Then he added: Shall I tell you of the essence of the matter, its pillar, and its peak? I replied: Yes, O Messenger of Allah. He said: The essence of this matter is Islam, its pillar is the prayer, and its peak is Jihad. Then he said: Shall I tell you of what holds all these things? I said: Yes, O Messenger of Allah. He took hold of his tongue and said: Keep this under control. I asked: O Prophet of Allah, shall we be held accountable for what we say? He replied: May your mother lose you! What else can cast people on their faces—or on their noses—except the harvest of their tongues?!"

Maelezo

Amesema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, siku moja nikawa karibu naye tukiwa tunatembea, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nieleze amali itakayoniingiza Peponi na kuniweka mbali na moto, akasema: Bila shaka umeuliza kuhusu jambo kubwa kulifanya kwake katika nafsi, na bila shaka ni jepesi na ni rahisi mno kwa atakayerahisishiwa na Mwenyezi Mungu kulifanya; tekeleza faradhi za Uislamu; Ya kwanza: Umuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala usimshirikishe na chochote. Ya pili: Usimamishe swala tano za faradhi mchana na usiku: Alfajiri, Adhuhuri, Alasiri, Magharibi, Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Ya tatu: Utoe zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya wajibu kwa kila mali iliyofikia kiwango katika sheria, na wanapewa wastahiki wake. Ya nne: Ufunge mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na mengineyo katika mambo yenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama kwa Jua. Ya tano: Utaizuru nyumba kwa kwenda Makka ili kutimiza ibada, kwa lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je nikufahamishe kuhusu njia inayokufikisha katika milango ya heri? Nayo ni kwa kutekeleza faradhi na sunna hizo: Ya kwanza: Ni funga ya hiyari, nayo inamzuia mtu kuingia katika maasi, nayo ni kwa kuvunjavunja matamanio, na kuzidhoofisha nguvu. Ya pili: Sadaka ya kujitolea inazima madhambi baada ya kuyafanya na huyaondosha na kufuta athari zake. Ya tatu: Swala ya tahajudi katika theluthi ya mwisho ya usiku, kisha akasoma rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hunyanyuka mbavu zao" Yaani: Hujiweka mbali, na "malazi" Yaani: Mahali pa kulala, "wakimuomba Mola wao Mlezi" Yaani: kwa swala na dhikri na kusoma Qur'ani na dua, "kwa hofu na tamaa, na katika yale tuliyowaruzuku wanatoa, hakuna nafsi ijuayo yale waliyofichiwa, katika yale yenye kutuliza macho" Yaani: Yale yenye kutuliza macho yao siku ya Kiyama na katika pepo miongoni mwa neema, "ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyafanya". Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikueleze msingi wa dini? na nguzo yake inayosimamia? na kiini cha kilele chake? Akasema Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake: Ndio, nieleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kichwa cha mambo yote ni: Uislamu nao ni shahada mbili, na kwa shahada hizi mbili ndio mtu anapata msingi wa dini. Na nguzo yake: Ni swala, hakuna Uislamu bila swala, kama ambavyo nyumba haiwezi kusimama pasina nguzo, atakaye swali dini yake itakuwa na nguvu na itanyanyuka; Na kiini cha kilele chake na kimo chake ni Jihadi na kutoa juhudi katika kupambana na maadui wa dini ili kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hivi nikuelezeni umadhubuti na ufanisi wa yaliyopita? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akashika ulimi, na akasema: Zuia huu na wala usizungumze yale yasiyokuhusu. Akasema Muadhi: Je atatuchukulia makosa na kutuhesabu Mola wetu Mlezi na kutuadhibu kwa kila tunachozungumza?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Amekupoteza mama yako! Na makusudio yake si kumuombea dua mbaya, bali ni katika maneno ya waarabu yaliyokuwa yakitumika kumtanabahisha mtu kuwa jambo hili unatakiwa kulichukulia tahadhari kubwa na kulielewa, kisha akasema; na unadhani ni kipi kitawatupa watu na kuwadondosha kwa nyuso zao ndani ya moto zaidi ya chumo za ndimi zao, ikiwemo ukafiri na kumzulia mtu machafu na matusi na utesi na usengenyaji, na uongo na mfano wa hayo.

Faida

  • Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kutaka kujifunza, na ndio maana maswali yao yalikuwa ni mengi sana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Utambuzi wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao kwa kujua kwao kuwa matendo ni sababu ya kuingia Peponi.
  • Swali lililotoka kwa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake ni swali zito; kwa sababu kwa uhalisia ndio siri ya uhai na uwepo wa kila kitu, kila kilichopo katika dunia kwanzia wanadam au majini lengo lake la mwisho ima iwe Pepo, ama motoni, na ndio maana swali hili likawa zito.
  • Kuingia kwake peponi kumefungamanishwa na kuzitekeleza nguzo tano za Uislamu, nazo ni: Shahada mbili na swala na zaka na swaumu na Hija.
  • Kichwa cha dini na jukumu ghali na wajibu mkubwa ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kwa kumuabudu yeye peke yake asiye na mshirika.
  • Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa kuwafungulia milango ya kheri ili wajiongezee sababu za malipo na kusamehewa madhambi.
  • Fadhila za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa ibada za sunna baada ya kutekeleza faradhi.
  • Swala katika Uislamu ni sawa na nguzo linayosimamia hema, Uislamu unaondoka kwa kudondoka kwake, kama linavyodondoka hema kwa kudondoka kwa nguzo.
  • Ulazima wa kuhifadhi ulimi kwa yale yanayomdhuru mtu katika dini yake.
  • Kuuzuia ulimi na kuudhibiti na kuufunga ndio msingi wa kheri zote.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)