Kulingania Dini na Kujitolea
SOMO · Musnad Ahmad · Na. HE-66197

Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake

Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya

Kiarabu

عَنْ حُذَيْفَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّهَا سَتَكُونُ أُمَرَاءُ يَكْذِبُونَ وَيَظْلِمُونَ، فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَأَعَانَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَلَيْسَ مِنَّي، وَلَسْتُ مِنْهُ، وَلَا يَرِدُ عَلَيَّ الْحَوْضَ، وَمَنْ لَمْ يُصَدِّقْهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَلَمْ يُعِنْهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَهُوَ مِنِّي، وَأَنَا مِنْهُ، وَسَيَرِدُ عَلَيَّ الْحَوْضَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake, na wala hatokunywa katika Hodhi langu, na ambaye hatowaamini kwa uongo wao na akawa hakuwasaidia katika dhulma yao, basi huyo yuko miongoni mwangu, na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu".

English translation

Hudhayfah (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There will be rulers who tell lies and oppress; whoever believes their lies and assists them in their oppression does not belong to me, and I do not belong to him, and he will not come to the Hawd (Basin). But whoever does not believe their lies and does not assist them in their oppression belongs to me, and I belong to him, and he will come to the Hawd."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba watatawala watu baada ya kifo chake viongozi wanaosema uongo katika mazungumzo yao wanasema wasiyoyatenda, na wanadhulumu katika hukumu, atakayeingia kwao na akawasadikisha kwa uongo wao, au akawasaidia kufanya dhulma au kuitamka, kama kutoa majibu kwa lengo la kujipendekeza kwao na kutaraji mazuri waliyonayo; basi mimi niko mbali naye na yeye si miongoni mwangu, wala hatokuja katika Hodhi la mto Kauthari siku ya Kiyama, na ambaye hatoingia kwao na kuwasadikisha kwa uongo wao na kuwasaidia juu ya dhulma yao basi huyo ni miongoni mwangu na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu siku ya Kiyama.

Faida

  • Watawala watu wakiingia kwao kwa lengo la kuwaelekeza na kuwapa nasaha na kupunguza shari; jambo hili ndilo linalotakiwa, ama wakiingia kwao kwa lengo la kuwasaidia katika dhulma na kuwasadikisha katika uongo hili ndilo jambo baya.
  • Kumebainishwa ahadi ya adhabu kali kwa atakayemsaidia kiongozi katika dhulma yake.
  • Ahadi hii katika hadithi inaonyesha uharamu wa kitendo hiki, na kuwa ni katika madhambi makubwa.
  • Himizo la kusaidizana katika wema na uchamungu, na kutosaidizana katika madhambi na uadui.
  • Kumethibitishwa Hodhi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba Umma wake utakunywa hapo.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)