Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 1977

Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَيْسَ الْمُؤْمِنُ بِالطَّعَّانِ وَلاَ اللَّعَّانِ وَلاَ الفَاحِشِ وَلاَ البَذِيءِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini si msemaji watu vibaya wala mtoaji wa laana wala muovu wala mwenye kauli chafu"

English translation

‘Abdullāh ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A believer is not a slanderer, nor a curser, nor a person who speaks obscenely, nor a person who uses foul language."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa si katika mambo ya muumini mwenye imani kamili kuwa mtoa aibu za watu katika nasaba zao, wala mwingi wa matusi na laana, wala muovu wa vitendo na kauli ambaye hana haya.

Faida

  • Kukanushwa imani katika dalili za kisheria hakuwi isipokuwa kwa kutenda kitendo cha haram au kuacha wajibu.
  • Himizo la kuhifadhi viungo na kuvilinda na mabaya, hasa hasa ulimi.
  • Amesema As-Sanadi: Na katika tamko la kusisitiza katika kauli yake (Mwingi kutukana, na mwingi wa kutoa laana) Ni dalili kuwa kutoa matusi na laana mara chache si vibaya kwa mtu atakayestahiki hilo, na wala haidhuru mtu kusifika kwa sifa za waumini.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)