Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika
Hukumu za Swala na Tohara
Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمْ المَسْجِدَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ اعْصِمْنِي مِنْ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ»، وَلِلْحَاكِمِ: «وَإِذَا خَرَجَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ أَجِرْنِي مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika, (Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: Allaahumma'swimnii minash-shaitwaanir-rajiim", (Ewe Mwenyezi Mungu nikinge dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Na katika riwaya ya Al-Haakim: "Na akitoka amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu nilinde dhidi ya Shetani aliyelaaniwa".
English translation
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (ﷺ) said: "When any of you enters the mosque, let him send peace upon the Prophet and say: Allāhumma iftahli abwāba rahmatik (O Allah, open for me the gates of Your mercy). And when he leaves, let him send peace upon the Prophet and say: Allāhumma i‘simni min ash-shaytān ar-rajīm (O Allah, protect me from the accursed devil)." In another narration by Al-Hākim: "When he leaves, let him send peace upon the Prophet (ﷺ) and say: Allāhumma ajirni min ash-shaytān ar-rajīm (O Allah, save me from the accursed devil)."
Maelezo
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Muislamu atakapotaka kuingia Msikitini amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusema: Allaahumma swalli alaa Muhammadi, kisha aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako". Na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na shetani aliyelaaniwa", na katika riwaya nyingine ya imamu Hakim: Na aseme: "Awe Mwenyezi Mungu nilinde na Shetani aliyelaaniwa".
Faida
- Sunna ya kusoma dua hii wakati wa kuingia Msikitini na wakati wa kutoka.
- Dua hii ni kwa misikiti yote, hata Msikiti mtukufu wa Makka.
- Rehema zimetajwa maalumu wakati wa kuingia, na kukingwa na Shetani wakati wa kutoka: Ni kwakuwa mwenye kuingia anashughulika na kile kinachomuweka karibu na Mwenyezi Mungu na karibu na Pepo yake ikawa ni mahala pazuri pa kutaja rehema, na akitoka anakwenda katika dunia na yote yaliyomo miongoni mwa mapumbao na vyenye kushughulisha, ikawa ni sehemu nzuri ya kuomba ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuhifadhiwa kutokana na Shetani.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.