Muslim — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih Muslim · Na. 994

Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ ثَوْبَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَفْضَلُ دِينَارٍ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ، دِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى عِيَالِهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ عَلَى دَابَّتِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى أَصْحَابِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ» قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَبَدَأَ بِالْعِيَالِ، ثُمَّ قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَأَيُّ رَجُلٍ أَعْظَمُ أَجْرًا مِنْ رَجُلٍ يُنْفِقُ عَلَى عِيَالٍ صِغَارٍ، يُعِفُّهُمْ أَوْ يَنْفَعُهُمُ اللهُ بِهِ وَيُغْنِيهِمْ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.

English translation

Thawbān (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The best dinar a man spends is a dinar that he spends on his dependents, and a dinar that a man spends on his mount in the cause of Allah, and a dinar that he spends on his companions in the cause of Allah." Abu Qilābah said: He began with the dependents. Then Abu Qilābah said: No man is greater in reward than a man who spends on young dependents, by virtue of whom Allah makes them chaste, or brings them benefit and enriches them.

Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aina za matumizi, na akazipanga pale panapokuwa na namna nyingi za kutoa matumizi kulingana na kile ambacho ni wajibu zaidi kwako, hivyo alianza na muhimu zaidi na kisha muhimu zaidi. Akaeleza kuwa mali yenye malipo mengi ni ile anayoitoa muislamu kwa wale anaolazimika kuwahudumia; kwanzia mkewe na watoto, kisha kutoa katika kipando kilichoandaliwa kwa ajili vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuwahudumia jamaa zake na rafiki zake wanapokuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Mpangilio wa matumizi katika ubora ni kwa namna ulivyotajwa, lizingatiwe hilo panapokuwa na majukumu mengi.
  • Kumebainishwa umuhimu wa kuanza na familia katika kutoa matumizi, na ndiko kuna fadhila nyingi kuliko kutoa sehemu zingine.
  • Kuhudumia Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni katika kutoa kukubwa, kama kuandaa vifaa na watu kwa ajili ya Jihadi.
  • Inasemekana kuwa: Makusudio ya njia ya Mwenyezi Mungu ni kila jambo la ibada, mfano kama Hija.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)