Qur'ani Tukufu na Fadhila Zake
SOMO · Sunan an-Nasa'i · Na. HE-65054

Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma

Usomaji na Kufanyia Kazi Qur'ani

Kiarabu

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «يقالُ لصاحبِ القرآن: اقرَأ وارتَقِ، ورتِّل كما كُنْتَ ترتِّل في الدُنيا، فإن منزِلَكَ عندَ آخرِ آية تقرؤها».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Amr (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said: "It will be said to the one devoted to the Qur’an: Read, ascend, and recite with deliberation as you used to recite in the world. Your rank will be at the last verse you recite."

Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifadhi, akiingia Peponi ataambiwa: Isome Qur'ani na upande cheo na daraja katika daraja za peponi, na usome kama vile ulivokuwa ukisoma Duniani kwa kuisoma kwa upole na utulivu; kwa hakika Cheo chako kitaishia kwenye Aya ya mwisho utakayo isoma.

Faida

  • Malipo huwa kwa mujibu wa matendo, kwa kuangalia wingi wake na namna yalivyofanywa.
  • Himizo juu ya kuisoma Qur'ani kwa namna nzuri na kuihifadhi na kuizingatia pamoja na kuifanyia kazi.
  • Pepo ina vituo na daraja nyingi, watu wa Qur'ani hupata daraja la juu kabisa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)