Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 390

Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ ابْنِ بُحَيْنَةَ رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبْطَيْهِ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Maliki bin Buhaina radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake.

English translation

Abdullah ibn Mālik ibn Buhaynah (may Allah be pleased with him) reported: When the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) prayed, he used to spread out his hands until the whiteness of his armpits would be visible.

Maelezo

Alikuwa rehema na amani zimshukie anaposwali, anaikunjua mikono yake wakati wa kusujudu. Alisogeza kila mkono kutoka upande wa karibu yake, kama mbawa mbili, mpaka rangi ya ngozi ya makwapa yake inaonekana; Hii ni katika kupitiliza kuitanua mikono na kuitenganisha na mbavu zake.

Faida

  • Mkao huu unapendeza katika sijida, nao ni kuweka mbali vikwapa na mbavu.
  • Maamuma ambaye jirani yake anakereka kwa kutanua kwake mikono; si sheria kwake kufanya hivyo.
  • Katika kutanua mikono katika sijida, kuna hekima na faida nyingi, miongoni mwake ni: kuonyesha uchangamfu na hamu ya kusali, na kwamba ikiwa mtu ataegemea viungo vyote katika sijida, kila kiungo kitapata sehemu yake ya ibada. Ikasemwa kuwa: Hekima katika hili ni kuwa ni sawa na unyenyekevu, na inafaa zaidi katika kuweka paji la uso na pua karibu na ardhi, na pia ili kila kiungo kiweze kutofautishwa peke yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)