Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 5139

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: مَنْ أَبَرُّ؟ قَالَ: «أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أَبَاكَ، ثُمَّ الْأَقْرَبَ فَالْأَقْرَبَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".

English translation

Bahz ibn Hakīm reported from his father from his grandfather that he said: I said: O Messenger of Allah, to whom should I be dutiful? he said: "Your mother, then your mother, then your mother, then your father, then the next in nearness and so on."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na kuishi naye vizuri, na kusuhubiana naye na kumuunga: Ni mama, na akasisitiza haki ya mama zaidi kuliko mtu mwingine, kwa kulirudia hilo mara tatu; kwa kubainisha fadhila zake kuliko watu wengine bila kupunguza chochote. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake anayefuata katika kutendewa wema: Kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kila ndugu anavyozidi kuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi ya kuungwa udugu kuliko ndugu wa mbali.

Faida

  • Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.
  • Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.
  • Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)