Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 1520

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنِينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّهَا قَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَرَى الجِهَادَ أَفْضَلَ العَمَلِ، أَفَلاَ نُجَاهِدُ؟ قَالَ: «لَا، لَكُنَّ أَفْضَلُ الجِهَادِ: حَجٌّ مَبْرُورٌ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."

English translation

‘Ā’ishah, Mother of the Believers, (may Allah be pleased with her) reported saying: O Messenger of Allah, we consider Jihad the best deed; should we not perform Jihad? He said, "No; rather, the best Jihad is Mabrūr (accepted) Hajj."

Maelezo

Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi? Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).

Faida

  • Jihadi ni katika amali bora kwa wanaume.
  • Haji kwa wanawake ni bora kuliko Jihadi, na ni miongoni mwa matendo bora kwao.
  • Amali zinazidiana ubora na zinatofautiana kulingana na mfanyaji.
  • Hija inaitwa Jihad; Kwa sababu ni Jihadi kwa ajili ya nafsi, na inahusisha kutoa mali na nguvu ya mwili, hivyo ni ibada ya mwili na mali kama kupigana Jihadi kwa ajili ya Allah.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)