Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-10897

Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَتَبَاهَى النَّاسُ فِي الْمَسَاجِدِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".

English translation

Anas (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "The Hour will not be established until people boast about mosques."

Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Uharamu wa kujifaharisha kwa Misikiti, na kwamba ni jambo lisilokubalika; kwa sababu kitendo hicho hakikufanyika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  • Katazo la kuipamba Misikiti kwa rangi na vito na nakshi, na maandishi; kwa sababu ndani yake kuna kuwashughulisha wenye kuswali wanapoyatazama.
  • Amesema Assanadi: Hadithi ni miongoni mwa zile ambazo uhalisia unashuhudia yaliyosemwa, ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)