Fiqhi, Swala na Ibada
SOMO · Sunan Ibn Majah · Na. HE-8357

Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu

Hukumu za Swala na Tohara

Kiarabu

عَن عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْمَاءِ وَمَا يَنُوبُهُ مِنَ الدَّوَابِّ وَالسِّبَاعِ، فَقَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا كَانَ الْمَاءُ قُلَّتَيْنِ لَمْ يَحْمِلِ الْخَبَثَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".

English translation

‘Abdullah ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) was asked about water that is frequented by animals and beasts of prey, and he (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "If the water is two pitchers, it will bear no impurity."

Maelezo

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.

Faida

  • Maji yananajisika ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake, au harufu yake, na hadithi imeeleza kwa ujumla na si kwa kuweka kikomo.
  • Wamekubaliana wanachuoni kuwa maji yakibadilishwa na najisi basi yananajisika moja kwa moja, sawa sawa yawe kidogo au mengi.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)