Hadithi na Sunnah za Mtume ﷺ
SOMO · Sahih Muslim · Na. HE-6982

Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo

Umuhimu wa Kufuata Sunnah

Kiarabu

عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدَبٍ وَالْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنهما قَالَا: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَدَّثَ عَنِّي بِحَدِيثٍ يُرَى أَنَّهُ كَذِبٌ، فَهُوَ أَحَدُ الْكَاذِبِينَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"

English translation

Samurah ibn Jundab and Al-Mughīrah ibn Shu‘bah (may Allah be pleased with both of them) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever reports a Hadīth on my authority that is thought to be false is one of the two liars."

Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayenukuu Hadithi kutoka kwake hali yakuwa anajua au anadhani au dhana yake kubwa kuwa ni kumzulia uongo rehema na amani ziwe juu yake; basi mpokezi atashirikiniana na mwanzilishi wa uongo huu katika dhambi.

Faida

  • Kuzichunguza hadithi zinazopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kupata uhakika wa usahihi wake kabla ya kuzipokea na kuzisimulia.
  • Sifa ya uongo ataitwa kila aliyezusha uongo na kwa yule atakayeuhamisha na kuusambaza kwa watu wengine.
  • Ni haramu kusimulia Hadithi ya uzushi kwa mtu anayejua kuwa ni ya kutunga, au anayedhania kuwa ni ya kutunga, isipokuwa kama ni kwa ajili ya kutahadharisha.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)