Aqidah na Misingi ya Imani
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. HE-6763

Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho

Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu

Kiarabu

عن عبد الله بن عكيم رضي الله عنه مرفوعاً: «مَنْ تَعَلَّقَ شيئا وُكِلَ إليه».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".

English translation

‘Abdullāh ibn ‘Akīm (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever is attached to something will be entrusted to that thing."

Maelezo

Atakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.

Faida

  • Katazo la kuegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Ulazima wa kuegemea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
  • Kubainishwa madhara ya ushirikina na ubaya wa mwisho wake.
  • Malipo huendana na matendo.
  • Nikuwa malipo ya kitendo hurudi kwa mfanyaji yakiwa ya kheri au ya shari.
  • Kushindwa kwa mwenye kujiondoa kwa Mwenyezi Mungu na akatafuta manufaa kwa asiyekuwa yeye.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)