Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا مِنْ مُسْلِمَيْنِ يَلْتَقِيَانِ فَيَتَصَافَحَانِ إِلَّا غُفِرَ لَهُمَا قَبْلَ أَنْ يَفْتَرِقَا».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Barraa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana".
English translation
Al-Barā’ (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "No two Muslims meet and shake hands except that their sins are forgiven before they part."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hakuna waislamu wawili watakaokutana njiani na mfano wake wakasalimiana kwa kupeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana kwa viwiliwili au kwa kumaliza kupeana mikono.
Faida
- Sunna ya kupeana mikono wakati wa kukutana, na himizo juu yake.
- Amesema Manawi: Na sunna haipatikani isipokuwa kwa kuweka mkono wa kulia katika mkono wa kulia kiasi kwamba hakuna udhuru.
- Himizo la kusambaza salamu, na kumebainishwa ukubwa wa malipo ya kumpa mkono muislamu ndugu yake muislamu.
- Kunavuliwa katika hadithi kupeana mikono kwa haramu, kama kumpa mkono mwanamke wa kando.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.