Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَسُبُّوا الرِّيحَ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مَا تَكْرَهُونَ فَقُولُوا: اللَّهُمَّ إِنَّا نَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ الرِّيحِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا وَخَيْرِ مَا أُمِرَتْ بِهِ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ هَذِهِ الرِّيحِ وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُمِرَتْ بِهِ».
Tafsiri ya Kiswahili
Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa".
English translation
’Ubayy ibn Ka‘b (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Do not curse the wind. If you see what you dislike, then say: Allāhumma inna nas’aluka min khayri hādhihi ar-rīh wa khayri ma fīha wa khayri ma ’umirat bih, wa na’ūdhu bika min sharri hādhihi ar-rīh wa sharri ma fīha wa sharri ma ’umirat bih (O Allah, we ask you for the good of this wind, the good that is in it, and the good that it has been commanded to bring; and we seek refuge with You from the evil of this wind, the evil that is in it, and the evil it has been commanded to bring)."
Maelezo
Amekataza rehema na amani ziwe juu yake kuutukana au kuulani upepo, kwani umeamrishwa kutoka kwa muumba wake, huja kwa rehema na adhabu, na kuutukana ni kumtukana Mwenyezi Mungu muuba wake, na kuchukia maamuzi yake, kisha akaelekeza rehema na amani ziwe juu yake kurejea kwa Mwenyezi Mungu muumba wake kwa kumuomba kheri zake na kheri zilizo ndani yake, na kheri za yale yaliyotumwa, kama kuleta mvua na kuchevusha mimea na mfano wake, na kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake na shari zilizo ndani yake, na shari zilizotumwa, kama kuharibu mimea na miti na kuangamiza mifugo na kubomoa majengo, na mfano wake, na katika kumuomba Mwenyezi Mungu hilo kuna kutimiza na kuthibitisha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Faida
- Katazo la kutukana upepo; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hapo matusi yanarudi kwa muumbaji wake na mpangiliaji wake, nayo ni mapungufu katika tauhidi.
- Kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuomba kinga kwake kutokana na shari ya vile alivyoumba.
- Upepo huamrishwa kwa kheri, na huamrishwa kwa shari.
- Amesema bin Baazi: Kuutukana upepo ni miongoni mwa maasi; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hutumwa kwa kheri na shari; haifai kuutukana, na wala haitakiwi kusema: Mwenyezi mungu aulaani upepo, au Mwenyezi Mungu auangamize upepo, Mwenyezi Mungu asiubariki upepo huu, au mfano wa hayo, bali muumini anafanya yale aliyoelekezwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Yanalinganishwa na upepo katika uharamu wa kushutumu na kutukana yanayohusu joto na baridi na jua na vumbi na mengineyo katika yale ambayo ni katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na uendeshaji wake.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.