Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. 1482

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتَحِبُّ الْجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ.

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo.

English translation

‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) liked comprehensive supplications and would leave aside anything else.

Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua zenye kukusanya kheri za dunia na Akhera ambazo matamshi yake ni machache na maana yake ni nyingi, na kunakuwa ndani yake na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na malengo mazuri, na anaachana na yasiyokuwa hayo.

Faida

  • Kupendeza kuomba dua kwa matamshi machache yenye kukusanya maana nyingi za kheri, na karaha ya kujikalifisha na kujitia tabu katika kuomba, jambo ambalo ni kinyume na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipendelewa kwa kuwa na maneno machache yenye kukusanya maana pana.
  • Kupupia yaliyothibiti kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kwa maombi hayo; hata kama dua ikiwa ndefu, na maneno yake yakawa mengi, yote ni katika dua zilizokusanya maana pana.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)