Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 2018

Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ جَابِرٍ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ مِنْ أَحَبِّكُمْ إِلَيَّ وَأَقْرَبِكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ القِيَامَةِ أَحَاسِنَكُمْ أَخْلاَقًا، وَإِنَّ أَبْغَضَكُمْ إِلَيَّ وَأَبْعَدَكُمْ مِنِّي مَجْلِسًا يَوْمَ القِيَامَةِ الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ وَالمُتَفَيْهِقُونَ»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، قَدْ عَلِمْنَا الثَّرْثَارُونَ وَالمُتَشَدِّقُونَ فَمَا الْمُتَفَيْهِقُونَ؟ قَالَ: «الْمُتَكَبِّرُونَ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika katika watu wanaopendeka zaidi kati yenu kwangu mimi, na atakayekaa karibu zaidi kati yenu na mimi siku ya Kiyama ni yule atakayekuwa na tabia njema zaidi kati yenu, na hakika ninaowachukia zaidi kati yenu na watakaokaa mbali zaidi na mimi siku ya Kiyama ni watu wenye maneno mengi, na waropokaji, na wenye kujifakharisha, wakasema: Tushajua maana ya watu wenye maneno mengi na waropokaji, nini maana ya wenye kujifakharisha? Akasema: "Ni wale wenye kiburi".

English translation

Jābir (may Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Indeed, among the most beloved to me and the closest of you to me in position on the Day of Judgment are those of you who have the best morals, and, indeed, the most hated of you to me and the farthest from me in position on the Day of Judgment are the talkative, the pompous, and the Mutafayhiqūn." They said: O Messenger of Allah, we know the talkative and the pompous, but who are the Mutafayhiqūn? He said: "The arrogant."

Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa miongoni mwa wale wanaowapendeka zaidi kati yenu kwake katika dunia, na wa karibu zaidi katika kikao miongoni mwenu siku ya Kiyama, ni yule mwenye tabia nzuri zaidi yenu, na kuwa anayechukiwa zaidi miongoni mwenu kwake katika dunia, na atakayekuwa mbali zaidi miongoni mwenu katika kikao siku Kiyama ni mwenye tabia mbaya zaidi miongoni mwenu; "Wenye maneno mengi" wenye kukithirisha maneno kwa kukijilazimisha na kwa kutoka katika haki, "na wenye kuzama zaidi" wenye kuzungumza maneno kwa upana kwa kujitia ufasaha na kwa kuyatukuza maneno yao pasina kuchukua tahadhari wala kuchunga, "na wenye kujitia kujua" wakasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwisha wajua wenye maneno mengi na wenye kuzama zaidi, ni wapi wenye kujifanya kujua? Akasema: Ni wenye kiburi wenye kuwakejeli watu, wale wenye kuzungumza kwa upana katika maneno yao, na hufungua vinywa vyao kwa wingi wa maneno.

Faida

  • Tabia njema ni miongoni mwa sababu za kupendwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kuwa karibu naye siku ya Kiyama, na tabia mbaya ni kinyume na hivyo.
  • Tabia njema ni miongoni mwa sababu za watu kupendana wao kwa wao, na tabia mbaya kinyume na hivyo.
  • Himizo la kuwa na tabia njema na unyenyekevu na kutokuwa na ususuwavu na kujikalifisha.
  • Tahadhari ya kuzungumza kwa wingi na kiburi na kujikweza na kujikalifisha.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)