Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Sunan Abu Dawud · Na. HE-5479

Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّعَاءُ لاَ يُرَدُّ بَيْنَ الأَذَانِ وَالإِقَامَةِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".

English translation

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Supplication between the Adhān (call to prayer) and the Iqāmah (second call to prayer) is not rejected."

Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.

Faida

  • Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.
  • Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
  • Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.
  • Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)