Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu
Wema, Uadilifu na Tabia Njema
Kiarabu
عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا شَيْءٌ أَثْقَلُ فِي مِيزَانِ الْمُؤْمِنِ يَوْمَ القِيَامَةِ مِنْ خُلُقٍ حَسَنٍ، وَإِنَّ اللَّهَ لَيُبْغِضُ الفَاحِشَ البَذِيءَ».
Tafsiri ya Kiswahili
Kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".
English translation
Abu ad-Dardā’ (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There is nothing heavier on the believer's scale on the Day of Judgment than good morals. Indeed, Allah detests the one who is indecent and foulmouthed."
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama katika kauli na matendo ni tabia njema, na hii ni kwakuwa na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi, na kutenda wema. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anamchukia mtu muovu katika kauli zake na vitendo, mwenye mdomo mchafu katika yale yanayotamkwa na ulimi wake.
Faida
- Ubora wa tabia njema; kwa sababu humletea mwenye nayo mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na mapenzi ya waja wake, nalo ndilo jambo kubwa katika yale yatakayopimwa siku ya Kiyama.
Jifanyie mazoezi
Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.