Bukhari — bado haijapangwa (ya muda)
SOMO · Sahih al-Bukhari · Na. 394

“Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.”

Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda)

Kiarabu

عَنْ أَبِي أَيُّوبَ الأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا أَتَيْتُمُ الغَائِطَ فَلاَ تَسْتَقْبِلُوا القِبْلَةَ، وَلاَ تَسْتَدْبِرُوهَا وَلَكِنْ شَرِّقُوا أَوْ غَرِّبُوا» قَالَ أَبُو أَيُّوبَ: فَقَدِمْنَا الشَّأْمَ فَوَجَدْنَا مَرَاحِيضَ بُنِيَتْ قِبَلَ القِبْلَةِ فَنَنْحَرِفُ، وَنَسْتَغْفِرُ اللَّهَ تَعَالَى.

Tafsiri ya Kiswahili

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

English translation

Abu Ayyūb al-Ansāri (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "When you go to a place to relieve yourselves, do not face or turn your back to the Qiblah (prayer direction); rather, turn towards the east or the west." Abu Ayyūb said: We came to the Levant and found lavatories built in the direction of the Qiblah, so, we used to divert ourselves and ask forgiveness from Allah Almighty.

Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kutaka kukidhi haja kubwa au ndogo kuelekea Kibla na upande wa Al-Kaaba, na asiigeuze kwa kuiweka nyuma ya mgongo wake. Bali ni lazima ageuke akiwa ndani kuelekea Mashariki au Magharibi ikiwa Kibla chake ni kama kibla cha watu wa Madina. Kisha Abuu Ayub (radhi za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa walipofika Sham walikuta vyoo vilivyotayarishwa kwa ajili ya kujisaidia vimejengwa kuelekea Al-Kaaba, hivyo wakawa wakijigeuza kutoka upande wa Kibla, pamoja na hivyo bado wanamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.

Faida

  • Hekima ya kufanya hilo ni kuitukuza Al-Kaaba tukufu na kuiheshimu.
  • Kuomba msamaha kwa Allah baada ya kutoka mahali pa kukidhi haja.
  • Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; Kwa sababu alipoeleza lililokatazwa akaelekeza linalofaa.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)