Maadili, Adabu na Tabia Njema
SOMO · Jami' at-Tirmidhiy · Na. 3591

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya

Wema, Uadilifu na Tabia Njema

Kiarabu

عَن قُطْبَةَ بنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ مُنْكَرَاتِ الأَخْلاَقِ وَالأَعْمَالِ وَالأَهْوَاءِ».

Tafsiri ya Kiswahili

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na tabia mbaya na matendo mabaya, na matamanio mabaya"

English translation

Qutbah ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) used to say: "Allāhumma inni a‘ūdhu bika min munkarāti al-akhlāqi wal-a‘māli wal-ahwā’ (O Allah, I seek refuge with You from evil morals, deeds, and desires)."

Maelezo

Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga" Yani: Ninaomba ulinzi na ukaribu "kwako" na si kwa asiyekuwa wewe, "kutokana tabia mbovu" alizozikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake, "katika tabia" kama chuki na husuda na kiburi, "na" mabaya "katika matendo" kama kutukana na kushutumu, "na" yote "matamanio", ambayo nafsi inayatamani hali yakuwa yanakwenda kinyume na sheria.

Faida

  • Ubora wa dua hii na kujibiwa kwake.
  • Muumini anapupia kuepuka tabia mbaya na matendo maovu, na anachukua tahadhari ya kufuata matamanio na kutumbukia katika matamanio.
  • Kugawanyika kwa tabia na matendo na matamanio katika maovu na mazuri.

Jifanyie mazoezi

Ficha maneno kisha jaribu kusoma kutoka kichwani. Bonyeza neno lililofichwa ili kuliona.

Fungua usomaji kamili (sauti)