Nyuma

Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّكُمْ تَقْرَؤُونَ هَذِهِ الآيَةَ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا عَلَيْكُمْ أَنْفُسَكُمْ لاَ يَضُرُّكُمْ مَنْ ضَلَّ إِذَا اهْتَدَيْتُمْ}، وَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوْا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمُ اللَّهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ».

Kutoka kwa Abubakari Swiddiq, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, ya kwamba yeye alisema: Enyi watu! Hakika nyinyi mnasoma aya hii: "Enyi mlioamini lililo lazima juu yenu ni nafsi zenu hatokudhuruni aliyepotoka ikiwa mtaongoka", na hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika watu wakimuona dhalimu na wasimchukulie hatua, basi wako karibu Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wote kwa adhabu yake."

Abu Bakr as-Siddīq (may Allah be pleased with him) reported: O people, you recite this verse: {O you who believe, take care of your own selves. Those who have gone astray will not harm you as long as you are guided.} Indeed, I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "When people see an oppressor but do not stop him, Allah will soon overwhelm them with a punishment from Him."

Ni wajibu wa Waislamu kuusiana na kuamrishana mema na kukataza maovu.

Adhabu ya jumla ya Mwenyezi Mungu inajumuisha dhalimu kwa udhalimu wake, na inajumuisha yule ambaye kakaa kimya na kutomkemea ikiwa ana uweza wa kukemea.

Kutoa mafunzo ya jumla na kuwaelewesha jumbe za Qur’ani kwa njia sahihi.

Ni lazima mtu achunge kukielewa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ili asikielewe kwa namna tofauti na vile alivyokusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Uongofu haupatikani ikiwa mtu ataacha kuamrisha mema na kukataza maovu.

Tafsiri sahihi ya Aya nikuwa: Shikamaneni na kuzihifadhi nafsi zenu na maasi, mtakapozihifadhi nafsi zenu hakutokudhuruni kupotea kwa aliyepotea ikiwa mtashindwa kuamrisha mema na kukataza maovu, kwa kuyaendea kwake makatazo, pale mtakapoongoka nyinyi kuyaepuka hayo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Jami' at-Tirmidhiy · Hadith Na. 2168 (Kulingania Dini na Kujitolea · Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
tirmidhi:he:3470