Nyuma

Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِمُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ، حِينَ بَعَثَهُ إِلَى الْيَمَنِ: «إِنَّكَ سَتَأْتِي قَوْمًا أَهْلَ كِتَابٍ، فَإِذَا جِئْتَهُمْ فَادْعُهُمْ إِلَى أَنْ يَشْهَدُوا أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللهَ قَدْ فَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ بِذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ، وَاتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ، فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ».

Imepokelewa Kutoka kwa bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Alisema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Muadhi Ibn Jabal, alipomtuma kwenda Yemen: "Hakika wewe utaiendea jamii ya watu wa kitabu (Mayahudi na Wakristo), utakapowajia basi waite kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao swala tano katika kila usiku na mchana, ikiwa watakutii kwa hilo, basi waeleze kuwa Mwenyezi Mungu amewalazimisha juu yao zaka, huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafukara wao, ikiwa watakutii kwa hilo, basi jiepushe na mali zao za thamani, na ogopa maombi ya mwenye kudhulumiwa, kwani maombi hayo hayana baina yake na Mwenyezi Mungu kizuizi".

Ibn ‘Abbās (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) said to Mu‘ādh ibn Jabal as he was sending him to Yemen: "You will come to a people of the Scripture. When you reach them, invite them to testify that none is worthy of worship except Allah and that Muhammad is the Messenger of Allah. If they obey you in that, tell them that Allah has enjoined on them five prayers every day and night. If they obey you in that, tell them that Allah has enjoined Zakah on them, to be taken from the rich amongst them and given to the poor amongst them. If they obey you in that, beware of taking their best properties; and fear the invocation of an oppressed person, for there is no barrier between his invocation and Allah.”

Maana ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, ni kumfanya Allah kuwa wa pekee kwa ibada, na kuacha kuabudu visivyokuwa Yeye.

Maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Ni kumuamini yeye na yale aliyokuja nayo na kumsadikisha, nakuwa yeye ni wa mwisho katika Wajumbe wa Mwenyezi Mungu kuja kwa wanadamu.

Nikuwa kujadiliana na msomi mwenye hoja tata si sawa na kujadiliana na mjinga; Ndio maana alimtanabahisha Muadhi kwa kumwambia: "Hakika wewe unakwenda katika jamii ya watu wa kitabu".

Kuna umuhimu wa muislamu kuwa na uelewa katika dini yake; ili asalimike na upotovu wa wenye kumtia utata, na hii inakuwa kwa kutafuta elimu.

Ubatili wa dini ya Mayahudi na Wakristo baada ya kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa wao si miongoni mwa watakao okoka siku ya Kiyama mpaka waingie katika dini Uislamu, na wamuamini Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 1496 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:3390