Nyuma

Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَن عَبدِ الله بنِ الشِّخِّير رضي الله عنه قَالَ: انْطَلَقْتُ في وَفدِ بَنِي عَامِرٍ إِلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقُلنا: أَنتَ سيّدُنَا، فقال: «السَّيدُ اللهُ»، قُلنا: وَأَفْضَلُنا فَضْلاً، وأعظَمُنا طَوْلاً، فقال: «قُولُوا بِقَولِكُم، أَو بَعضِ قولِكُم، وَلَا يَسْتَجْرِيَنَّكُم الشَّيطَانُ».

Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Shikhiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".

‘Abdullah ibn ash-Shikhkhīr (may Allah be pleased with him) reported: I set out with the delegation of Banu ‘Āmir to meet the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). We said: You are our master. He said: "The Master is Allah." We said: And the best of us in superiority and the greatest among us in bounty. He said: "Say what you have to say, or part of what you have to say, but do not let the devil deviate you (in praising me)."

Utukufu wa cheo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndani ya nafsi za Masahaba wake na heshima yao kwake.

Katazo la kijikalifisha katika matamshi, na kubakia katika maneno yaliyozoeleka.

Kuilinda tauhidi dhidi ya yale yanayoiharibu miongoni mwa kauli na matendo.

Katazo la kuchupa mipaka katika kusifu, kwani hilo ni katika njia za Shetani.

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye bwana wa watoto wa Adam, na haya yaliyotajwa katika hadithi hii ni katika sehemu ya unyenyekevu, na ni katika sehemu ya kuwahofia wao wasijekuchupa mipaka katika hilo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sunan Abu Dawud · Hadith Na. 4806 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
abudawud:he:3389