Nyuma

Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi na aitafute katika siku saba za mwisho

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رِجَالًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُرُوا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي المَنَامِ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرَى رُؤْيَاكُمْ قَدْ تَوَاطَأَتْ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَمَنْ كَانَ مُتَحَرِّيهَا فَلْيَتَحَرَّهَا فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ».

Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba kuna baadhi ya watu katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walionyeshwa Lailatul qadri ndotoni katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi na aitafute katika siku saba za mwisho".

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: Some men among the Companions of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) were shown the Night of Qadr in their dreams to be in the last seven. The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "I see that your visions have agreed on the last seven, so, whoever seeks it, let him seek it in the last seven."

Ubora wa Lailatul-Qadri na himizo la kuitafuta.

Miongoni mwa hekima za Mwenyezi Mungu na huruma yake aliuficha usiku huu ili watu waongeze juhudi katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.

Usiku wa Lailatul-Qadri uko katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na katika siku saba za mwisho ndio hutarajiwa zaidi.

Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.

Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kiambata na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 2015 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:4545