Nyuma

Tulikuwa tukitoa kipindi alipokuwa nasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul fitiri, kwa kila mdogo na mkubwa, huru au mamluki, kibaba cha chakula, au kibaba cha siyagi, au kibaba cha ngano, au kibaba cha zabibu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا نُخْرِجُ إِذْ كَانَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ، عَنْ كُلِّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ، حُرٍّ أَوْ مَمْلُوكٍ، صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ، فَلَمْ نَزَلْ نُخْرِجُهُ حَتَّى قَدِمَ عَلَيْنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ أَبِي سُفْيَانَ رضي الله عنه حَاجًّا، أَوْ مُعْتَمِرًا فَكَلَّمَ النَّاسَ عَلَى الْمِنْبَرِ، فَكَانَ فِيمَا كَلَّمَ بِهِ النَّاسَ أَنْ قَالَ: إِنِّي أَرَى أَنَّ مُدَّيْنِ مِنْ سَمْرَاءِ الشَّامِ، تَعْدِلُ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، فَأَخَذَ النَّاسُ بِذَلِكَ، قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: فَأَمَّا أَنَا فَلَا أَزَالُ أُخْرِجُهُ كَمَا كُنْتُ أُخْرِجُهُ، أَبَدًا مَا عِشْتُ.

Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tukitoa kipindi alipokuwa nasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul fitiri, kwa kila mdogo na mkubwa, huru au mamluki, kibaba cha chakula, au kibaba cha siyagi, au kibaba cha ngano, au kibaba cha zabibu, hatukuacha kuendelea kuitoa, mpaka alipokuja kwetu Muawia bin Abii Sufian radhi za Allah ziwe juu yake kwa ajili ya Hija, au Umra, akazungumza na watu katika Mimbari, ikawa katika yale aliyozungumza na watu alisema kuwa: Hakika mimi ninaona kuwa vibaba viwili vya kipimo cha kutoka Samraa ya Sham, vinalingana na kibaba kimoja cha tende, watu wakalichukua hilo, anasema Abuu Saidi: Ama mimi niliendelea kuitoa kama nilivyokuwa nikiitoa, milele kwa muda wote nilioishi.

Abu Sa‘īd al-Khudri (may Allah be pleased with him) reported: When the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) was among us, we used to give out Zakat al-Fitr on behalf of every young and old person, free or slave, as one Sā‘ of food, or one Sā‘ of Aqit (dried yogurt), or one Sā‘ of barley, or one Sā‘ of dates, or one Sā‘ of raisins. We continued giving it out until Mu‘āwiyah ibn Abi Sufyān (may Allah be pleased with him) came to us for Hajj or ‘Umrah. He addressed the people from the pulpit, and among the things he said to the people was: Verily, I see that two Mudds of the Syrian wheat are equivalent to one Sā‘ of dates. So, people started applying this. Abu Sa‘īd said: As for me, I will continue to give it as I used to give it for as long as I live.

Kumebainishwa kiwango cha zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kibaba cha chakula hata kama aina na kiwango vitatofautiana.

Kila chakula cha binadam kinafaa kutoa zakatul-fitiri, bali zilitajwa aina nne pekee; kwa sababu ndicho kilikuwa chakula cha watu kwa zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Kutoa kisichokuwa chakula kama pesa, hakutoshelezi zakatul-fitiri.

Amesema Nawawi katika Sherehe ya Muslim: Na wakihitilafiana Maswahaba na kukawa hakuna kauli inayoonyesha kuwa kauli ya baadhi yao ni bora kuliko nyingine, tunarejea katika dalili nyingine, tutakuta kuwa dhahiri ya hadithi na kipimo cha akili vimekwenda sambamba katika kuweka sharti la kibaba cha ngano kuwa ni sawa na vibaba vingine, hivyo ni lazima kulifanyia kazi hilo.

Amesema bin Hajari: Na katika hadithi ya Abuu Saidi inaonyesha namna alivyokuwa na mkazo sana katika kufuata na kushikamana na mafundisho, na kuacha kuyavuka kwenda katika jitihada hali yakuwa mafundisho yapo, na katika kitendo cha Muawia na watu kuafikiana naye, ni dalili ya kufaa jitihada, nalo ni jambo zuri, lakini kukiwa na mafundisho jitihada zitakuwa mbovu na wala hazitozingatiwa.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 985 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:4454