عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ لِي قَرَابَةً أَصِلُهُمْ وَيَقْطَعُونِي، وَأُحْسِنُ إِلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إِلَيَّ، وَأَحْلُمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ، فَقَالَ: «لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ، فَكَأَنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ وَلَا يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nina ndugu wa karibu, ninawaunga lakini wao wananitenga, ninawafanyia wema lakini wao wanatendea ubaya, na ninakuwa mpole kwao lakini wao wananifanyia ujeuri, basi akasema: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo".
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: A man said: O Messenger of Allah, I have relatives with whom I maintain kinship ties, but they sever them with me; I treat them kindly, but they mistreat me; I tolerate them, but they are intolerant with me. He said: "If you are as you say, then it is as if you are feeding them hot ashes, and you will continue to have a supporter against them from Allah as long as you continue to do this."
Kuukabili ubaya kwa wema ni sehemu ya kumfanya muovu arejee katika haki, kama alivyosema Mtukufu: "Zuia (ubaya) kwa lile lililo jema, punde yule ambaye baina yako na yeye kuna uadui atakuwa kama rafiki mwandani"
Kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu hata kama kutatokea maudhi ni sababu ya kupata msaada wa Mwenyezi Mungu kwa mja muumini.
Kukata udugu ni maumivu na ni adhabu katika dunia, na ni madhambi na hesabu siku ya Kiyama.
Ni wajibu kwa muislamu ataraji malipo katika amali yake njema, na wala yasimkatishe maudhi ya watu na kumtenga kwao kukamuachisha ibada yake nzuri.
Si muunga udugu yule anayelipa wema wa yule aliyemuunga udugu, lakini muunga udugu wa kweli ni yule ambaye ukikatwa udugu wake yeye anauunga.