Nyuma

Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «اللهُمَّ لَا عَيْشَ إِلَّا عَيْشُ الْآخِرَهْ، فَاغْفِرْ لِلْأَنْصَارِ وَالْمُهَاجِرَهْ».

Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakuna maisha bora isipokuwa maisha ya Akhera, basi wasamehe Maanswari (watu wa Madina) na Muhajirina (waliohama kutoka kutoka Makkah)".

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "By Allah, there is no true life except that of the Hereafter, so forgive the Ansār (Supporters) and the Muhājirah (Emigrants)."

Kutoipenda kwake Dunia rehema na amani ziwe juu yake na kuilekea kwake Akhera.

Kuuepushia Mtume rehema na amani ziwe juu yake umma wake na kupenda starehe za Dunia zenye kuondoka.

Kumebainishwa nafasi ya Muhajirina na Answari, kiasi kwamba walibahatika kupata dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwaombea msamaha.

Mja hafurahii yale anayoyapata katika Dunia kwani huondoka upesi pamoja nakuwa na mateso makubwa, bali nyumba ya makazi ya kudumu ni Akhera.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 6414 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:3773