عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قَالَ اللَّهُ: كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ لَهُ، إِلَّا الصِّيَامَ، فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ، وَالصِّيَامُ جُنَّةٌ، وَإِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ فَلاَ يَرْفُثْ وَلاَ يَصْخَبْ، فَإِنْ سَابَّهُ أَحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ، فَلْيَقُلْ إِنِّي امْرُؤٌ صَائِمٌ، وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَخُلُوفُ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ المِسْكِ، لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ يَفْرَحُهُمَا: إِذَا أَفْطَرَ فَرِحَ، وَإِذَا لَقِيَ رَبَّهُ فَرِحَ بِصَوْمِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa, na swaumu ni kinga, na itakapokuwa ni siku ya kufunga mmoja wenu basi asitamke machafu, wala asifanye fujo, na ikiwa kuna mtu atamtukana au akampiga, basi aseme, mimi nimefunga, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hakika harufu ya mdomo wa mfungaji ni nzuri mno mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko harufu ya Miski, mfungaji anafuraha mbili anazofurahia: Anapofuturu hufurahi, na akikutana na Mola wake atafurahi kwa swaumu yake"
Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Allah said: All the deeds of the son of Adam are for himself except for fasting, as it is, indeed, for Me, and I give reward for it. Fasting is a shield. When it is the day when any of you is fasting, let him not engage in obscenity, and let him not speak in a loud voice. If anyone insults him or fights with him, let him say: Verily, I am a fasting person. By the One in Whose Hand the soul of Muhammad is, the smell of the mouth of the fasting person is more pleasant in the sight of Allah than the smell of musk. The fasting person will rejoice twice: when he breaks his fast, he rejoices, and when he meets his Lord, he rejoices at his fast."
Fadhila za swaumu nakuwa inamuhifadhi mfungaji katika dunia kutokana na matamanio, na Akhera kutokana na adhabu ya Moto.
Miongoni mwa adabu za swaumu ni kuacha maneno mabaya na ya hovyo, na kusubiri dhidi ya maudhi ya watu na kukabiliana na maudhi hayo kwa subira na ihisani.
Swaumu au mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu anapofurahi kwa sababu ya kukamilisha ibada yake na kuimaliza hilo halipunguzi malipo yake Akhera.
Furaha kamili inakuwa kwa kukutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, pale wanapotimiziwa wenye subira na wafungaji malipo yao pasina hesabu.
Kuwafahamisha watu kwa ibada uliyonayo wakati wa haja na masilahi si katika riyaa kwa kauli yake: "Hakika mimi nimefunga".
Mfungaji iliyekamilika swaumu yake ni yule viliyefunga viungo vyake kutokana na madhambi, na ulimi wake kutokana na uongo na machafu, na kusema uongo, na tumbo lake kutokana na chakula na vinywaji.
Katazo la kufanya fujo na ugomvi na zogo wakati wa swaumu limetiwa mkazo, lakini pia yamekatazwa hayo kwa mtu asiyekuwa katika swaumu.
Hadithi hii ni katika yale anayoyapokea Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithi ya kiuungu, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake imetoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina mambo maalumu kama ya Qur'ani ambayo inatofautiana kwayo na maneno mengine, ikiwemo kukitumia kisomo chake kama ibada na kuwa twahara (msafi) na kutoa changamoto na maswala kisayansi na mengineyo.