عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي: نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِي الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِي المَغَانِمُ، وَلَمْ تَحِلَّ لِأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu. Nimenusuriwa na hofu kwa umbali wa safari ya mwezi mmoja. Na nimefanyiwa ardhi kuwa mahali pa kuswalia na ni twahara (safi). Hivyo, yeyote katika umma wangu atakapokutwa na swala, basi na aswali (popote). Na nimehalalishiwa ngawira. Na kila Nabii alikuwa akitumwa kwa umma wake tu, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote. Na nimepewa uombezi (Siku ya Kiyama)”.
Jābir ibn ‘Abdullah (may Allah be pleased with him and his father) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "I was granted five that none before me was granted: I was granted victory through terror from a distance of one month's journey; the earth has been made for me a mosque and a means of purification, so any man from my Ummah who is caught up by the prayer should pray; the spoils of war have been made lawful for me, although they were not lawful for anyone before me; I have been granted the intercession; and a prophet used to be sent to his people in specific, whereas I have been sent to all people."
Sheria ya mtu kuhesabu neema za Mwenyezi Mungu juu yake kwa kuzisimulia na kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
Fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umma huu na kwa Nabii wao, kwa kupewa mambo haya.
Uwajibu wa kuitekeleza swala kwa wakati wake kwa hali yoyote ile itakayokuwa, na mtu afanye awezacho katika sharti zake na nguzo zake na wajibu wake.
Utetezi maalumu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake unaotofautiana na wa Manabii, una aina nyingi: Ya kwanza: Utetezi wake kwa viumbe ili hukumu ipite baina yao, na pia: Utetezi wake wa kuingia watu wa peponi peponi, na pia: Utetezi wake maalumu kwa ami yake Abii Twalib katika kupunguziwa adhabu ya moto si kutolewa kwenye moto; kwa sababu alikufa kafiri.
Mambo ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni mengi mno ambayo hayakutajwa katika hadithi hii yakiwemo: Alipewa mkusanyo wa maneno (maneno machache yenye maana pana), na umehitimishwa utume kupitia kwake, na zimefanywa safu zetu kuwa kama safu za Malaika, na mambo mengine mengi.