Nyuma

Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: نَظَرْتُ إِلَى أَقْدَامِ الْمُشْرِكِينَ عَلَى رُءُوسِنَا وَنَحْنُ فِي الْغَارِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ لَوْ أَنَّ أَحَدَهُمْ نَظَرَ إِلَى قَدَمَيْهِ أَبْصَرَنَا تَحْتَ قَدَمَيْهِ، فَقَالَ: «يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا ظَنُّكَ بِاثْنَيْنِ اللهُ ثَالِثُهُمَا».

Kutoka kwa Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliitazama miguu ya washirikina juu ya vichwa vyetu, na sisi tukiwa pangoni, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: "Ewe Abubakari, kwani ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao".

Abu Bakr as-Siddīq (may Allah be pleased with him) reported: When we were in the cave, I saw the feet of the polytheists as I raised my head, and I said: O Messenger of Allah, if one of them looked below his feet, he would see us. He said: "O Abu Bakr, what do you think of two persons, the third of whom is Allah?"

Nafasi ya Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake kwa kuambatana kwake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuhama kwake kutoka Makka kwenda Madina, na kutengena kwake na familia yake na mali yake.

Huruma ya Abubakari radhi za Allah ziwe juu yake, na kiwango cha mapenzi yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hofu yake kwake dhidi ya maadui.

Uwajibu wa kuwa na imani na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutulizana katika ulinzi wake na himaya yake, baada ya kutumia juhudi katika kukwepa na kuchukua tahadhari.

Mwenyezi Mungu kuwajali Manabii wake na Mawalii wake, na kuwalinda kwa kuwapa ushindi, amesema Mtukufu: "Hakika sisi tunawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakaposimama mashahidi".

Angalizo kuwa yeyote atakayemtegemea Mwenyezi Mungu basi atamtosheleza, na atamnusuru, na atamsaidia, na atamlinda na atamuhifadhi.

Ukamilifu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wa kumtegemea Mola wake Mlezi, na kwamba yeye anategemea kwake, na anakabidhi kwake mambo yake.

Ushujaa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuzituliza kwake nyoyo na nafsi.

Kukimbia kwa ajili ya dini kwa kumuogopa adui, na kuchukua sababu za kuokoka.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2381 (Historia na Wasifu wa Mtume ﷺ · Maisha ya Mtume na Maswahaba)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:3447