Nyuma

Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الذَّهَبُ بِالذَّهَبِ، وَالْفِضَّةُ بِالْفِضَّةِ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ، وَالْمِلْحُ بِالْمِلْحِ، مِثْلًا بِمِثْلٍ، سَوَاءً بِسَوَاءٍ، يَدًا بِيَدٍ، فَإِذَا اخْتَلَفَتْ هَذِهِ الْأَصْنَافُ، فَبِيعُوا كَيْفَ شِئْتُمْ، إِذَا كَانَ يَدًا بِيَدٍ».

Kutoka kwa Ubada bin Swaamit -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono".

‘Ubādah ibn as-Sāmit (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Gold for gold, silver for silver, wheat for wheat, barley for barley, dates for dates, and salt for salt, like for like, equal for equal, hand to hand. If these classes differ, sell as you wish if it is hand to hand."

Kumebainishwa mali zinahusika katika riba na namna ya kuuza ndani yake.

Katazo la kuuza kwa riba.

Fedha za noti au sarafu zinachukua hukumu ya dhahabu na fedha katika sababu ya riba yake.

Kuuza na kununua aina hizi sita zenye kuhusika katika riba kuna hali nyingi: 1- Ni kuuzwa riba kwa riba kwa aina hiyo hiyo, kama dhahabu kwa dhahabu na tende kwa tende.... na ni sharti kusihi kwake kuwe na sharti mbili: 1- Kufanana katika uzani au kilo, na kukabidhiana katika kikao cha makubaliano, 2- Ni kuuzwa riba kwa riba kwa aina tofauti ikiwa ni pamoja na kufanana kwa sababu, kama dhahabu kwa fedha, na ngano isiyokobolewa kwa ngano iliyokobolewa, ni sharti kuwe na kukabidhiana, pasina kufanana, 3- Ni kuuza riba kwa riba kwa aina tofauti ikiwa ni pamoja na kutofautiana sababu, katika hilo hakuna sharti la kukabidhiana, wala mfanano kama kuuza dhahabu kwa tende.

Kuuza na kununua aina zisizokuwa na uhusiano na riba, au moja wake ikawa ni ya riba na nyingine si riba; na ni sharti katika hilo kukabidhiwa, na wala hakuna sharti la kufanana, kama kuuza jengo kwa dhahabu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 1587 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:66385