Nyuma

Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَادمِ اللَّذَّاتِ» يَعْنِي الْمَوْتَ.

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo.

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Remember the destroyer of pleasures frequently," meaning death.

Kifo kinakata ladha za dunia, lakini kwa muumini kinamuhamisha kwenda katika ladha za Akhera na ladha za pepo na yale yanayopatikana ndani yake miongoni mwa kheri kubwa.

Kukumbuka kifo na yale yanayokuwa baada yake ni miongoni mwa sababu za kutubia na kujiondoa katika dhambi na kujiandaa na Akhera.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Jami' at-Tirmidhiy · Hadith Na. HE-66232 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Ni nzuri (Hasan) · Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
tirmidhi:he:66232