Nyuma

Tahadharini na madhambi yenye kudharauliwa

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِيَّاكُمْ وَمُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ، فَإِنَّمَا مَثَلُ مُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ كَقَوْمٍ نَزَلُوا فِي بَطْنِ وَادٍ، فَجَاءَ ذَا بِعُودٍ، وَجَاءَ ذَا بِعُودٍ، حَتَّى أَنْضَجُوا خُبْزَتَهُمْ، وَإِنَّ مُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ مَتَى يُؤْخَذْ بِهَا صَاحِبُهَا تُهْلِكْهُ».

Kutoka kwa Sahal bin Sa'di Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini na madhambi yenye kudharauliwa, kwani mfano wa madhambi yenye kudharauliwa, ni kama watu walioshuka chini ya bonde, akaja huyu na kijiti, na yule na kijiti, na akaja huyu na kijiti, mpaka wakaivisha mkate wao, na bila shaka madhambi yadharauliwayo akihesabiwa mfanyaji wake yanamuangamiza".

Sahl ibn Sa‘d (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Beware of insignificant sins, for indeed, an example of insignificant sins is like a group of people who alighted at the bottom of a valley: one of them brought a stick, and another brought a stick, until they cooked their bread. Verily, insignificant sins, if one is held accountable for them, they perish him."

Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kupiga mifano ili kusogeza maana karibu ili kufahamika vizuri na kuongeza ubainifu zaidi.

Tahadhari ya madhambi madogo yenye kudharauliwa, na himizo la kwenda mbio ili kuyafuta.

Madhambi yenye kudharauliwa yanabeba maana nyingi: Maana ya kwanza: Ni yale anayoyafanya mja miongoni mwa madhambi, akidhani kuwa ni katika madhambi madogo, hali yakuwa ni katika madhambi makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ya pili: Ni yale anayoyafanya mja pasina kujali, na bila kutubia, yakakusanyika juu yake haya madogo mpaka yakamuangamiza. Na ya tatu: Ni yale anayoyafanya mja katika madhambi madogo, na asiyajali, yakawa ni sababu ya kutumbukia katika madhambi makubwa na yakamuangamiza.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-66224 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:he:66224