Nyuma

Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ أَحَبَّ أَسْمَائِكُمْ إِلَى اللهِ عَبْدُ اللهِ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ».

kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika majina yenu yanayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Abdullah na Abdul-Rahman".

Ibn ‘Umar (may Allah be pleased with him and his father) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Indeed, the dearest of your names to Allah is ‘Abdullah and ‘Abdur-Rahmān."

Amesema Al-Qurtubi: Yanaunganishwa na majina haya mawili yote yanayokuwa mfano wake kama Abdul-Rahiim, na Abdul-Maliki na Abdul-Swamad, na yamekuwa pendwa kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu yanaambatana na wasifu wa wajibu kwa Mwenyezi Mungu na wasifu kwa mwanadamu na ni wajibu kwake ambao ni utumwa, kisha mja akaambatanishwa kwa Mola Mlezi kuambatanishwa halisi, yakasadikisha majina haya, na yakapata utukufu kwa kuunganishwa huku, na yakapata fadhila hii, na wamesema wengineo: Hekima ya kufupisha kwa majina mawili ni kuwa haikuwahi kutokea kuambatanishwa ndani ya Qur'ani utumwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa majina haya mawili, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na kwamba pindi aliposimama mja wa Mwenyezi Mungu akimuomba" na akasema katika aya nyingine: "Na waja wa Al-Rahman (Mwingi wa rehema) na inaungwa mkono na kauli yake Mtukufu: "Sema muombeni Allah au muombeni Al-Rahmaan".

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2132 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:65978