عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: تَلَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ هَذِهِ الْآيَةَ: {هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ، وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ، وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ} [آل عمران: 7]. قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَإِذَا رَأَيْتِ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ سَمَّى اللهُ، فَاحْذَرُوهُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Aya hii :{Yeye ndiye ambaye alikuteremshia kitabu hiki ndani yake kuna Aya muhkam -zilizo wazi- aya hizo ambazo ndiyo msingi wa kitabu hiki na zipo nyingine zinatatiza, wale ambao nyoyoni mwao kuna upotofu watafuata zile zenye kutatiza kwa kutaka kufitinisha na kutaka kujua uhakika wa maana yake, na hakuna ajuaye uhakika wa maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wale wabobezi katika elimu wanasema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu na hawakumbuki isipokuwa wenye akili} (Al- imaraan 7) Anasema Aisha: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya"
‘Ā’ishah (may Allah be pleased with her) reported: The Prophet (may Allah’s peace and blessings be upon him) recited this verse: {It is He Who has sent down to you the Book. In it are definite verses, which are the foundation of the Book, while others are ambiguous. Those with deviant hearts follow the ambiguous verses, seeking discord and seeking their [false] interpretation. But no one knows their [true] interpretation except Allah. And those who are well-grounded in knowledge say: "We believe in it. It is all from our Lord." None will take heed except people of understanding} [Surat Āl ‘Imrān: 7]. Then, he said: "If you see those who follow the ambiguous verses, they are those whom Allah has named; so, beware of them."
Al-muhkam katika aya za Qur'ani: Ni zile ambazo ni nyepesi kuzifahamu maana zake zipo wazi, na zenye kutatiza ni zile zenye kuchukua zaidi ya maana moja na zinahitajia uchunguzi wa kina na ufahamu.
Kuchukua tahadhari ya kutochanganyikana na watu waliopotoka, na watu wazushi na wenye kuleta mambo yenye kutatiza kwa ajili ya kuwapoteza watu na kuwatia mashaka.
Katika kumalizia aya kwa maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili" Inaashiria kuwapinga wapotofu na kuwasifia waliojikita katika elimu, yaani asiyekumbuka wala kupata mawaidha, na akafuata matamanio ya nafsi yake huyo si miongoni mwa wenye kutumia akili.
Kufuata mambo yenye kutatiza ni sababu ya kuupotosha moyo.
Ni wajibu kuzirudisha aya ambazo maana zake zinatatiza na hazifahamiki maana zake, katika aya ambazo maana yake ni nyepesi kufahamika.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya baadhi ya aya kuwa ni nyepesi na zingine ni zenye kutatiza; Ili awajaribu watu na kuwapambanua wenye imani na watu waliopotea.
Kwa kutokea aya zenye kutatiza katika Qur'ani: Ni kudhihirisha ubora wa maulamaa kuliko watu wengine, na kuifahamisha akili kuhusu mapungufu yake; ili ijisalimishe kwa muumba wake na ikubali kushindwa kwake.
Ubora wa kujikita katika elimu na ulazima wa kudumu katika elimu.
Na maulamaa wa tafsiri kwenye kusimama katika neno (Allah) katika maneno yake aliposema {Wamaa ya'alamu taawilahuu illa llahu warraasikhuuna fil ilmi} kuna kauli mbili, kwa yule atakayesimama katika neno (Allah), basi yanakuwa makusudio ya neno Taawiil ni ujuzi wa uhakika wa kitu kwa namna ambayo hakuna njia ya kuujua, kama vile jambo linalohusu roho na kiyama katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha katika elimu yake, na wale wabobezi katika elimu wao wanaziamini na wanaegemeza uhakika wake kwa Mwenyezi Mungu, hivyo basi wanajisalimisha na wanasalimika, na mwenye kupitiliza bila ya kusimama kwenye neno( Allah) basi inakuwa maana ya neno Taawili ni tafsiri na kuweka wazi, hivyo inakuwa Mwenyezi Mungu anajua na waliobobea katika elimu vilevile wanajua, hivyo wanakuwa ni wenye kuziamini na wana zirudisha kwenye aya zilizo nyepesi.