Nyuma

"Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».

Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."

Zayd ibn Khālid al-Juhani (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah’s peace and blessings be upon him) led us in the Fajr prayer at Al-Hudaybiyah after rainfall during the night. At the conclusion of the prayer, he turned toward the people and said: "Do you know what your Lord has said?" They replied: "Allah and His Messenger know best." He said: "He has said: 'Some of My servants have entered the morning as believers in Me and some as disbelievers. He who says, 'We have had rainfall by the grace and mercy of Allah' believes in Me and disbelieves in the stars, and he who says, 'We have had rainfall by the rising of such and such star' disbelieves in Me and believes in the stars.'"

Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.

Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.

Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.

Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.

Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 71 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:65010