Nyuma

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: مَنْ أَبَرُّ؟ قَالَ: «أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أَبَاكَ، ثُمَّ الْأَقْرَبَ فَالْأَقْرَبَ».

Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".

Bahz ibn Hakīm reported from his father from his grandfather that he said: I said: O Messenger of Allah, to whom should I be dutiful? he said: "Your mother, then your mother, then your mother, then your father, then the next in nearness and so on."

Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.

Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.

Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-58188 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Ni nzuri (Hasan) · Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:he:58188