Nyuma

Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «سَتَكُونُ أَثَرَةٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «تُؤَدُّونَ الحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسْأَلُونَ اللَّهَ الَّذِي لَكُمْ».

Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu".

Ibn Mas‘ūd (may Allah be pleased with him) reported that the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There will be selfishness and other matters that you will disapprove of after me." They asked: What do you order us to do (in such circumstances), O Messenger of Allah? He said: '"Fulfill your duty (towards the ruler), and ask Allah for your rights."

Hadithi hii ni katika dalili za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake, kiasi ambacho alieleza mambo yatakayotokea ndani ya Umma wake na yakatokea kama alivyoeleza.

Inafaa kumueleza mtahiniwa yale yatakayomsibu katika mitihani; ili aitulize nafsi yake, mtihani ukimfika atakuwa na subira na atataraji malipo toka kwa Allah.

Kushikamana na Qur'ani na Sunna ni sababu ya kutoka katika fitina na hitilafu.

Himizo la kuwa wasikivu na watiifu kwa viongozi katika mema, na kutojitoa katika utiifu, hata kama zitatokea kwao dhulma.

Kutumia hekima na kufuata mafundisho ya Mtume wakati wa fitina.

Ni jukumu la kila mtu kutimiza haki ya msingi inayomlazimu hata kama itatokea kadhulumiwa.

Hadithi inaashiria kanuni ya msingi ambayo ni: Mtu kuchagua moja kati ya shari mbili au madhara yenye nafuu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 3603 (Bukhari — bado haijapangwa (ya muda) · Hadith zilizogunduliwa hivi karibuni (ya muda))
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili (jina la mtafsiri halijatajwa katika API) · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:hadeethenc-provisional:3156