Nyuma

Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ فِي صَلاَتِهِمْ»، فَاشْتَدَّ قَوْلُهُ فِي ذَلِكَ، حَتَّى قَالَ: «لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ».

Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao".

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: The Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "What is the matter with some people who raise their eyes towards the sky during their prayer?" He went on, using strict words, until he said, "They must stop that, or their eyesight will be snatched away."

Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kubainisha kwake haki; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake hakumtaja mkosefu; kwa sababu lengo ni kubainisha haki na tayari imekwisha tendeka; na kwa sababu ndani yake kuna kumsitiri mkosefu na inahamasisha zaidi mtu kukubali ukweli.

Katazo la msisitizo, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua macho yake juu mbinguni ndani ya swala.

Amesema katika kitabu cha Aunul Ma'buud: Na sababu katika hilo ni kwamba atakaponyanyua macho yake juu mbinguni atakuwa katoka katika nembo ya kibla na ameipuuza na katoka katika muonekano wa swala pia.

Kunyanyua macho kunaondoa utulivu ndani ya swala.

Ukubwa wa hadhi ya swala, na kwamba ni wajibu kwa wenye kusali wawe katika adabu kamili pamoja na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 750 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:10883