Nyuma

Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُقْبَةَ بْنَ عَامِرٍ الْجُهَنِيَّ رضي الله عنه قَالَ: ثَلَاثُ سَاعَاتٍ كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَانَا أَنْ نُصَلِّيَ فِيهِنَّ، أَوْ أَنْ نَقْبُرَ فِيهِنَّ مَوْتَانَا: حِينَ تَطْلُعُ الشَّمْسُ بَازِغَةً حَتَّى تَرْتَفِعَ، وَحِينَ يَقُومُ قَائِمُ الظَّهِيرَةِ حَتَّى تَمِيلَ الشَّمْسُ، وَحِينَ تَضَيَّفُ الشَّمْسُ لِلْغُرُوبِ حَتَّى تَغْرُبَ.

Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu: wakati linapoanza kuchomoza jua mpaka linyanyuke, na wakati linapofika kati kati mpaka lipinde, na wakati linapoanza kuzama mpaka lizame.

‘Uqbah ibn ‘Āmir al-Juhani (may Allah be pleased with him) reported: Three hours the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) used to forbid us from praying or burying our deceased ones in them: when the sun begins to rise until it has fully risen; when the sun is at its zenith until it begins to decline; and when the sun starts setting until it has fully set.

Nyakati zilizokatazwa kuswali ndani yake kama ilivyoonyesha hadithi hii na hadithi nyinginezo, nazo ni: Wa kwanza: Baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua linapochomoza. Wa pili: Wakati wa kuchomoza jua mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki kwa mtazamo wa jicho; yaani: kiasi cha dakika kumi na tano takribani. Wa tatu: Anaposimama msimamaji wa mchana mpaka jua liondoke, na hii ni wakati ambao unakuwa hakijabakia kivuli kwa mwenye kusimama mchana, upande wa Mashariki wala Magharibi, na wameukadiria baadhi yao kuwa ni dakika tano takribani. Wa nne: Baada ya swala ya Lasiri mpaka jua lizame. Wa tano: Wakati jua linapokuwa la njano mpaka lizame.

Katazo la kuswali katika nyakati hizi tano zilizokatazwa, zinaondolewa hapo swala za faradhi na swala zenye sababu.

Katazo la kuchelewesha kuzika mpaka katika nyakati hizi tatu zenye muda mfinyu zilizotajwa katika hadithi, na kufaa kwake katika nyakati nyinginezo sawa iwe mchana au usiku.

Hekima na maana ya kukataza kuswali ndani ya nyakati hizi: Asili ni nikuwa muislamu anajisalimisha kwa amri za Mwenyezi Mungu, na anajiepusha na makatazo yake kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na wala haachi kuabudu mpaka aone hekima au sababu ya kuamrishwa hivyo, au kukatazwa hilo, bali anatakiwa atii, na imekuja katika hadithi zingine hekima katika hilo: Ya kwanza: Nikuwa katika wakati wa mchana kabla ya kupinduka jua Jahanamu huwashwa muwako mkali. Ya pili: Na ama hekima ya kukatazwa swala wakati wa kuchomoza jua na wakati wa kuzama kwake, ni kujifananisha na washirikina, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza kwake na wakati wa kuzama kwake. Ya tatu: Na ama katazo la kuswali baada ya Alfajiri mpaka kuchomoza kwa jua, na baada ya Lasiri mpaka kuzama kwake, hii ni sehemu ya kuziba njia zinazopelekea katika mabaya; mpaka kumalizike kutojifananisha na makafiri, na waislamu wasijifananishe nao katika ushirikina wao, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza na wakati wa kuzama kwake.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 831 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:10604