Nyuma

hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنِ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها زَوْجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ الْحَوْلَاءَ بِنْتَ تُوَيْتِ بْنِ حَبِيبِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى مَرَّتْ بِهَا وَعِنْدَهَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: هَذِهِ الْحَوْلَاءُ بِنْتُ تُوَيْتٍ، وَزَعَمُوا أَنَّهَا لَا تَنَامُ اللَّيْلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَنَامُ اللَّيْلَ! خُذُوا مِنَ الْعَمَلِ مَا تُطِيقُونَ، فَوَاللهِ لَا يَسْأَمُ اللهُ حَتَّى تَسْأَمُوا».

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kwamba Haulaa binti Tuwaiti bin Habib bin Asadi bin Abdil-Uzza, alipita kwake akiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikasema: Huyu hapa Haulaa binti Tuwaiti, na wanadai kuwa huwa halali usiku, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake (kwa mshangao): "Halali usiku! hebu chukueni katika matendo kiasi mkiwezacho, na Wallahi ninaapa, Mwenyezi Mungu hachoki mpaka mchoke".

‘Ā’ishah, the Mother of the Believers (may Allah be pleased with her) and wife of the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him), reported: Al-Hawlā’ bint Tuwayt ibn Habīb ibn Asad ibn ‘Abdul-‘Uzza passed by while I was sitting with the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him). So I said: This is Al-Hawlā’ bint Tuwayt, and they claim that she does not sleep at night. Thereupon, the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "She does not sleep at night! Do what you are capable of doing (regularly). By Allah, Allah never grows weary (of giving rewards) until you grow weary (of doing good deeds)."

Kukithirisha kufanya ibada kwa zaidi ya kiwango unachoweza kuhimili mwili wa mtu hupelekea katika uchovu na kuelemewa na nafsi kuziacha.

Kuwa kati na kati katika utekelezaji wa ibada hupelekea kuendelea nazo na kudumu nazo.

Amali ndogo yenye kudumu ni bora kuliko nyingi yenye kukatika.

Amesema Nawawi: Kwa kudumu kiwango kidogo ibada huendelea kwa kuzikumbuka na kuzichunga, na kuwa na utakasifu wa nia na kumuelekea Mwenyezi Mungu, kinyume na ibada nyingi ngumu, kiasi ambacho hizi kidogo hupanda na kuongezeka na kuzidi hizi nyingi zilizokatika mara dufu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. HE-10411 (Kulingania Dini na Kujitolea · Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:10411