Nyuma

Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عن أنس بن مالك رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمُعَاذٌ رَدِيفُهُ عَلَى الرَّحْلِ قَالَ: «يَا مُعَاذُ بْنَ جَبَلٍ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، قَالَ: «يَا مُعَاذُ»، قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللهِ وَسَعْدَيْكَ، ثَلَاثًا، قَالَ: «مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللهُ عَلَى النَّارِ»، قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَفَلَا أُخْبِرُ بِهِ النَّاسَ فَيَسْتَبْشِرُوا؟ قَالَ: «إِذًا يَتَّكِلُوا». وَأَخْبَرَ بِهَا مُعَاذٌ عِنْدَ مَوْتِهِ تَأَثُّمًا.

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto", akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, je, niwaeleze watu ili wapate habari njema? Akasema: "Ukifanya hivyo, watabweteka". Na alieleza Muadhi jambo hili wakati wa kifo chake kwa kuogopa kupata dhambi za kuficha elimu.

Anas ibn Mālik (may Allah be pleased with him) reported: As the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) was riding a mount with Mu‘ādh behind him, he said: "O Mu‘ādh ibn Jabal!" He replied: "Here I am at your service, O Messenger of Allah." He again said: "O Mu‘ādh!" Mu‘ādh replied: "Here I am at your service, O Messenger of Allah." This was said three times. Then, the Prophet (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "There is no one who bears witness that there is no god but Allah and that Muhammad is His slave and Messenger, sincerely from his heart, except that Allah will make him forbidden to Hellfire." He said: "O Messenger of Allah, should I not inform the people of that so that they may rejoice?" He replied: "Then they would rely on this alone." Mu‘ādh narrated this Hadīth at the time of his death to avoid the sin of concealing knowledge.

Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumpakiza kwake Muadhi nyuma ya mnyama wake.

Njia ya ufundishaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba alirudia rudia wito kwa Muadhi ili akaze usikivu wake kwa yale atayoyazungumza.

Katika sharti za shahada: Ya Kushuhudia kuwa hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni awe msemaji wake ni mkweli na yakini, asiwe muongo au na shaka.

Watu wa tauhidi hawatokaa milele katika moto wa Jahannam, hata kama watauingia kwa sababu ya madhambi yao; watatolewa baada ya kusafishwa.

Fadhila za shahada mbili kwa atakayezisema akiwa mkweli.

Kufaa kuacha kuzungumza baadhi ya mazungumzo katika baadhi ya hali, yatakapoambatana na madhara.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih al-Bukhari · Hadith Na. 128 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
bukhari:he:10098