Nyuma

Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ بُرَيْدَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَلَفَ بِالْأَمَانَةِ فَلَيْسَ مِنَّا».

Kutoka kwa Buraida -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu".

Buraydah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever swears by the Amānah (trust) is not one of us."

Uharamu wa kuapa kumuapia asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwemo: Kuiapia amana, nakuwa hilo ni katika shirki ndogo.

Amana inakusanya utiifu na ibada, na kuwekeza, na pesa tasilimu, na amana.

Kiapo hakikubaliki ila kwa kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa jina miongoni mwa majina yake au kwa sifa katika sifa zake.

Amesema Al-Khattwabi: Hadithi inaonekana kuwa karaha hapa ni kwa sababu aliamrisha aape kwa Allah na kwa sifa zake, na amana si katika sifa zake, bali ni amri katika amri zake, na ni faradhi katika faradhi zake, wakakatazwa hilo kwakuwa ndani yake kuna kuifanya amana kuwa sawa na majina ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka na sifa zake.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Musnad Ahmad · Hadith Na. HE-8964 (Aqidah na Misingi ya Imani · Tawhid na Kumtii Mwenyezi Mungu)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa na Abu Daud na Ahmad
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
ahmad:he:8964