عَنْ هِشَامِ بْنِ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّهُ مَرَّ عَلَى أُنَاسٍ مِنَ الْأَنْبَاطِ بِالشَّامِ، قَدْ أُقِيمُوا فِي الشَّمْسِ، فَقَالَ: مَا شَأْنُهُمْ؟ قَالُوا: حُبِسُوا فِي الْجِزْيَةِ، فَقَالَ هِشَامٌ: أَشْهَدُ لَسَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ اللهَ يُعَذِّبُ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاسَ فِي الدُّنْيَا».
Kutoka kwa Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba yeye alipita kwa watu miongoni mwa Anbat huko Sham, wakiwa wamesimamishwa juani, akasema: Wamekuwaje? Wakasema: Wamefungwa kwa sababu ya jizia (kodi), akasema Hisham: Ninashuhudia kuwa nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani"
Hishām ibn Hakīm ibn Hizām (may Allah be pleased with him and his father) reported that while in the Levant, he passed by some Nabataean peasants who had been made to stand in the sun. He said: What is this? They said: They have been imprisoned on account of Jizyah (protection tax). So Hishām said: I testify that I heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "Verily, Allah tortures those who torture people in this world."
Jizia: Ni mali inayowekwa kuwa sheria kwa wanaume miongoni mwa Mayahudi na Manaswara waliobalehe wenye uwezo, kwa ajili ya kulindwa kwao na kuishi kwao katika mji wa kiislamu.
Uharamu wa kuwaadhibu watu hata makafiri, pasina kigezo cha kisheria.
Onyo kwa madhalimu kutokana na dhuluma.
Walishikamana Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kuamrisha mema na kukataza maovu.
Amesema Nawawi: Hii inachukuliwa katika kuadhibu bila haki, haiingii kuadhibu kwa haki kama kisasi, na kusimamishiwa sheria, na kuonya, na mfano wake.