Nyuma

Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na atakayesema kumwambia ndugu yake: Njoo tucheze kamari, basi na atoe sadaka

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَلَفَ فَقَالَ فِي حَلِفِهِ: وَاللَّاتِ وَالعُزَّى، فَلْيَقُلْ: لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَمَنْ قَالَ لِصَاحِبِهِ: تَعَالَ أُقَامِرْكَ، فَلْيَتَصَدَّقْ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na atakayesema kumwambia ndugu yake: Njoo tucheze kamari, basi na atoe sadaka".

Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "Whoever swears by Al-Lāt and Al-‘Uzza should say: 'There is no god but Allah'. And whoever says to his companion 'Come and gamble with me' should give charity."

Kiapo hakiwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake.

Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu, ama kuapa kwa masanamu kama Lata au Uzza au kuapia amana, au kuapa kwa Mtume au kitu kingine chochote.

Amesema Khattwabi: Kiapo kinakuwa kwa Muabudiwa Mtukufu, basi akiapa kwa Lata na mfano wa hayo anakuwa kawaiga makafiri, basi akaamrishwa kukirekebisha kwa neno la tauhidi.

Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu si lazima atoe kafara ya kiapo chake, bali anatakiwa kutubia na kuomba msamaha, kwa sababu hilo ni kubwa mno kuliko kusamehewa na kisichokuwa toba.

Kumeharamishwa kamari kwa aina zake zote na mitindo yake yote, ambayo ni kamari aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akaiambatanisha na pombe na masanamu.

Ulazima wa kurudi na kuacha maasi wakati wa kuyafanya.

Atakayefanya jambo baya anatakiwa afuatishe jambo jema; kwa sababu matendo mema huondoa maovu.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. HE-6379 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:6379