Nyuma

Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عُثْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَا مِنَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ تَحْضُرُهُ صَلَاةٌ مَكْتُوبَةٌ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهَا وَخُشُوعَهَا وَرُكُوعَهَا، إِلَّا كَانَتْ كَفَّارَةً لِمَا قَبْلَهَا مِنَ الذُّنُوبِ، مَا لَمْ يُؤْتِ كَبِيرَةً، وَذَلِكَ الدَّهْرَ كُلَّهُ».

kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".

‘Uthmān (may Allah be pleased with him) reported that he heard the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) say: "No Muslim person who, when an obligatory prayer becomes due, perfects its ablution, humility, and bowing except that it becomes an expiation for the sins that preceded it as long as he has not committed a major sin, and this applies to all times."

Swala inayofuta madhambi ni ile ambayo mja katawadha vizuri udhu wake, na akaitekeleza kwa unyenyekevu akitafuta radhi za Mwenyezi Mungu kwa swala hiyo.

Fadhila za kudumu katika ibada, nakuwa ibada ni sababu ya kusamehewa madhambi madogo.

Fadhila za kutawadha vizuri, na kuswali vizuri pamoja na utulivu ndani yake.

Umuhimu wa kuyaepuka madhambi makubwa ili kusamehewa madhambi madogo.

Madhambi makubwa hayafutwi ila kwa toba.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 228 (Fiqhi, Swala na Ibada · Hukumu za Swala na Tohara)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:6254