عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضيَ اللهُ عنها أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تُحِدُّ امْرَأَةٌ عَلَى مَيِّتٍ فَوْقَ ثَلَاثٍ إِلَّا عَلَى زَوْجٍ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا، وَلَا تَلْبَسُ ثَوْبًا مَصْبُوغًا إِلَّا ثَوْبَ عَصْبٍ، وَلَا تَكْتَحِلُ، وَلَا تَمَسُّ طِيبًا إِلَّا إِذَا طَهُرَتْ نُبْذَةً مِنْ قُسْطٍ أَوْ أَظْفَارٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Ummu Atwiya -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiache mapambo na kupendeza mwanamke yeyote kwa maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa mume wake atakaa miezi minne na siku kumi, na wala asivae nguo yenye urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, wala asipake wanja, wala asiguse manukato, isipokuwa atakapotwaharika anaweza kuchukua kiasi kidogo cha Qustwi au Adhfar (aina ya marashi ya kufukiza, hutumiwa na wanawake)".
’Umm ‘Atiyyah (may Allah be pleased with her) reported that the Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said: "A woman should not mourn for any dead person more than three days except her husband, for whom she should mourn four months and ten days. She should not wear dyed clothes (while in mourning) except ‘Asb (an unattractive Yemeni garment), nor should she apply kohl or touch perfume, except when she becomes purified (from her menses), as she may then apply a little Qust or Azhfār (types of incense)."
Ihdad maana yake: Ni kuacha urembo na mambo yanayochochea kumuoa, anatakiwa kuepuka mapambo yote, na marashi yote, na wanja, na aepuke nguo za mapambo.
Katazo la mwanamke kuacha urembo kwa sababu ya maiti zaidi ya siku tatu, isipokuwa mumewe.
Kumebainishwa nafasi ya mume kwa sababu hutakiwa kukaa eda kwa mwingine zaidi ya siku tatu.
Kuhalalishwa kuanzia siku tatu kushuka chini, kwa ajili ya kujifariji.
Ulazima wa mwanamke kuacha urembo kwa mumewe miezi minne na siku kumi, kama hatokuwa mjamzito, na akiwa hivyo basi mpaka atakapojifungua.
Anahalalishiwa nguo yenye mchanganyiko wa rangi isiyokuwa na urembo, na kigezo kinachotumika kuijua hapo ni kulingana na tamaduni za jamii yake.