Nyuma

Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale

Kisomo cha Kiarabu Kiarabu Fasaha (MP3)

عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قُلِ اللهُمَّ اهْدِنِي وَسَدِّدْنِي، وَاذْكُرْ بِالْهُدَى هِدَايَتَكَ الطَّرِيقَ، وَالسَّدَادِ سَدَادَ السَّهْمِ».

Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".

‘Ali (may Allah be pleased with him) reported: The Messenger of Allah (may Allah's peace and blessings be upon him) said to me: "Say: O Allah, guide me and make me adhere to the straight path, and when asking for Huda (guidance), think of your being guided to the right path, and Sadād (adherence to the straight path) is the straightness of the arrow."

Muombaji anatakiwa apupie kupatia katika amali yake na kuinyoosha kwa kushikamana na sunna na kutakasa nia.

Sunna ya kuomba dua kwa maneno haya yaliyokusanya kuwezeshwa na kusimamiwa katika mambo.

Ni wajibu kwa mja kutaka msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yake yote.

Kupiga mifano wakati wa kufundisha.

Kukusanya kati ya kutaka uongofu na kutengenezewa na hali, na kudumu juu yake na kutopotoka hata chembe ndogo na kutengemaa kwa mafikio, hivyo kauli yake: "Niongoze" Ili nitembee juu ya njia ya uongofu, na kauli yake: "Na unisimamie" ni katika kupatia na kutopotoka wakati wa uongofu uliomfika.

Muombaji anatakiwa aitilie maanani dua yake, na avute picha ya maana ya maombi yake ndani ya moyo wake; kwani hili huleta msukumo mkubwa wa kujibiwa dua.

Rejea na Daraja ya Hadithi

Kitabu na Mlango:
Sahih Muslim · Hadith Na. 2725 (Maadili, Adabu na Tabia Njema · Wema, Uadilifu na Tabia Njema)
Daraja na Mpokezi:
Sahihi · Imepokelewa Imamu Muslim
Mfasiri na Chanzo:
HadeethEnc.com — Kiswahili · Chanzo cha Tafsiri ↗
Masharti ya Matumizi:
Leseni ya Maudhui ↗
muslim:he:5915